Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imetoa msaada wa vyakula kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani kwa makundi maalumu ya wazee hapa visiwani Zanzibar.
Msaada huo unajumuisha sukari, unga wa ngano pamoja na mchele umetolewa katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo.
Kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar imeainisha wazee zaidi ya 120 wenye uhitaji wa vyakula kwenye mwezi huu wa Ramadhani walio chini ya jumuiya ya wazee hapa Zanzibar.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa wazee, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel-Zanzibar, bwana Mohammed Mussa, amesema ni kawaida kwa kampuni ya Zantel kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii katika kipindi hiki cha Ramadhani.

MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazee Zanzibar (JUWAZA), Mwadini Kutenga Haji akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa wazee wa Zanzibar uliotolewa na kampuni ya simu ya Zantel.
---
'Tuna furaha sana leo kuweza kusaidia jamii hii ya wazee ambao mara nyingi wamekuwa wanasahaulika, kwani tunaamini wazee ni sehemu muhimu sana ya jamii ndio maana Zantel leo tumeamua kutoa msaada huu ambao unatutofautisha sana na makampuni mengine katika vipaumbele vyetu' alisema Mussa.
Mussa aliongeza kuwa kama kampuni ya simu inayoongoza Zanzibar, Zantel mara zote

WAZEE mbali mbali wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vyakula uliotolewa na kampuni ya simu ya Zantel , makabidhiano hayo yalifanyika Kibanda maiti.
---
---
‘'Kwa misaada hii, Zantel
inawafanya wazee nao wajiskie sehemu ya jamii, kwani mara nyingi wamekuwa
wakisahaulika sana na kwa hakika hatutawasau kwa ukarimu wao huu'’ alisema bwana
Kutenga.
Kampuni ya Zantel imekuwa msitari wa mbele katika
kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani, na
msaada huu ni maalumu kwa kundi la wazee ambalo mara nyingi linasahaulika
katika jamii.
MKURUGENZI wa Biashara wa Kampuni ya simu ya Zantel ofisi ya Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza katika hafla ya kukabidhi misaada ya vyakula iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis akimkabidhi msaada , Pili Ahmada wakati wa makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Kampuni ya simu ya Zantel kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar, kulia Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti.
MZEE Hussein Abdalla akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis , msaada huo ulitolewa na kampuni ya simu ya Zantel, kulia Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti. (Picha na Haroub Hussein).

Toa Maoni Yako:
0 comments: