Klabu ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama ambazo zinamwezesha kila Mwanachama wa Simba kupata bima ya maisha hadi Tsh. 250,000 ikiwa atafiwa na mwenza au mtoto au yeye mwenyewe kupitia bima ya maisha iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba imezindua Kadi za watoto yaani Simba Clubs.
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akimkabidhi Mtoto Iqram Ally Kadi ya Simba Clubs waliyoizindua. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (kulia) Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange.


Toa Maoni Yako:
0 comments: