Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitoa huduma katika Banda la NSSF kwenye maonyesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuwahudumia wateja wao.
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitoa huduma katika Banda lao kwenye maonyesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuwahudumia wateja wao.
Kutoka kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Mafao ya Matibabu, Dk. Straton Simon na Nesi wa Hospitali ya Amana, Nuru Awadh (wa pili kushoto) wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la NSSF na kubahatika kupata huduma za afya bure.
Mmoja wa Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mbele aliyekaa akitoa huduma katika Banda lao kwenye maonyesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiwahudumia wateja wao.
Ofisa Mwandamizi wa Mafao ya Matibabu, Dk. Straton Simon (wa kwanza kushoto) pamoja na Nesi wa Hospitali ya Amana, Nuru Awadh (aliyevaa kofia) wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la NSSF na kubahatika kupata huduma za afya bure.
Kulia ni Meneja Kiongozi Masoko na Ushirikiano wa, Bi. Eunice Chiume akitoa ufafanuzi juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa mteja aliyetembelea banda hilo.
Kulia ni Meneja Kiongozi Masoko na Ushirikiano wa, Bi. Eunice Chiume akitoa ufafanuzi juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa mteja aliyetembelea banda hilo.
---
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linatoa huduma za afya bure kwa wateja mbalimbali watakaotembelea katika Banda la shirika hilo ndani ya Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Dar es Salaam ndani ya banda la NSSF Sabasaba, Ofisa Mwandamizi wa Mafao ya Matibabu, Dk. Straton Simon alisema shirika hilo limeamua kutoa huduma bure kwa wateja mbalimbali watakaowatembelea katika banda lao kwa muda wote wa maonesho hayo ili wajue afya zao na kupata ushauri kwa madaktari.
Dk. Simon alisema wameamua kutoa huduma za afya bure kwa magonjwa ambayo si ya kuambukiza na hayakupewa kipaumbele na Serikali kama ilivyo kwa magonjwa mengine ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha jamii kupenda kupima na kujua afya zao mara kwa mara. Aliongeza kuwa NSSF imeleta wataalamu wa vipimo pamoja na madaktari ambao wanaendesha zoezi hilo kwa wateja wanaowatembelea katika banda lao.
Alisema miongoni mwa vipimo ambavyo vinatolewa huduma ni pamoja na kuangalia shinikizo la damu (presha), kuangalia ugonjwa wa kisukari na kuangalia uwiano wa uzito na urefu kwa mteja kisha kupata nafasi ya kuonana na daktari moja kwa moja kujua matatizo ya mteja na kupata ushauri wa kitabibu na pia kuelezwa nini cha kufanya.
"...Tumeona ni vema kwenye kipindi hiki cha sabasaba tuweke huduma za afya ili kupima watu wote watakaopita kwenye banda hili...kuangalia urefu na uzito, baadaye tutapima presha yao, na sukari na hatimaye tunatoa ushauri kwa mteja juu ya nini cha kufanya na kama atakuwa na matatizo tunamuelekeza nini cha kufanya au pa kwenda kulingana na matatizo yake," alisema Dk. Simona katika ufafanuzi wake.


Toa Maoni Yako:
0 comments: