Kingunge Ngombale - Mwiru anakosea sana kumshambulia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kuhusu kwa kusimamia maamuzi ya vikao ndani kwani kazi ya Idara ya Itikadi na Uenezi ni kusimamia Itikadi na Uenezi. Kingunge na kundi lao wanashindwa kuona hata jina la hicho cheo?

Ni vyema tukajiuliza ni kitu gani kinachomsukuma Kingunge kupigana kufa na kupona kumtetea Edward Lowassa bila kuzingatia maslahi ya chama na taifa. Ni maslahi ya kibiashara, kifamilia ama?

Kwa nyakati tofauti, Nape alisema Kanuni za Uteuzi wa Wagombea wa CCM kuingia katika Vyombo vya Dola, toleo la Februari 2010 hazitoi nafasi kwa Mgombea wa Nafasi ya Uraisi kukata rufaa, kwani huko kutakuwa kurudi nyuma badala ya kwenda mbele.

Wajumbe wa NEC waliopo Dodoma wanasema baada ya kuanza kupoteza MATUMAINI, mkakati wa baadhi ya wagombea akiwamo Lowassa ni kuvuruga vikao visifanyike.

Wanasema huyo Lowassa aliwahi kukata rufaa huko nyuma, mwaka 1995 kwa kuwatumia makada Galus Abeid na Yusuf Makamba, lakini Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere, aliyesema kwamba kazi ya vikao vya maamuzi ni kupunguza idadi ya wagombea si kuongeza majina;

Mwaka 2005 Mzee John Samwel Malecela alikata rufaa kupinga kuenguliwa katika nafasi ya kuwania urais kupitia CCM na alipoomba kujieleza ndani ya NEC alijibiwa kwa dakika tatu tu kwa Mkapa kuzungumzia mambo mawili tu ikiwamo suala la umri kuwa mkubwa na kukumbushia kukataliwa kwa Malecela na Mwalimu Nyerere.

Katika mchakato huu unaoendelea sasa, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, alipoingizwa katika kundi la wataka urais sita waliosimamishwa na CCM mwaka 2014, aliamua kukata rufaa kupinga kuhukumiwa bila kuzingatia uzito wa makosa anayotuhumiwa nayo, lakini hadi sasa hakuwahi kujibiwa wala kujadiliwa na badala yake CCM iliendelea na mchakato wake.

Mjumbe Mmoja wa NEC mkongwe anasema katika hali ya kawaida, vikao vya maamuzi vinakuwa na ratiba ambayo wakiruhusu kukata rufaa, italazimika kusitisha shughuli zote kwa muda usiojulikana.

“Kinachofanywa na Kingunge ni kutafuta uhalali wa kutata rufaa ili kuvuruga mchakato, ili vikao vya NEC na Mkutano Mkuu usifanyike wakati Kanuni ya tano imekaa kimya kuhusu rufaa katika vikao vya uchujaji na uteuzi,” anasema.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mzee Kingunge anayeonekana kumtetea Lowassa alitoa mfano wa Mzee Malecela bila kueleza jinsi Mkapa alivyozima hoja ya Malecela alipopewa nafasi ya kuzungumza (si kwamba alikata rufaa) ndani ya NEC.

Tayari wafuasi wa Lowassa wameanza kueneza taarifa kwamba Nape amefukuzwa uongozi na kuvuliwa uanachama kwa kumzibia nafasi mgombea wao na kwamba mapendekezo hayo yametolewa na Kingunge, taarifa ambazo hazina ukweli wowote bali ni uzushi wa kujiliwaza wakijipa MATUMAINI.

Kingunge ambaye watu wengi wanaamini kwamba ni muumini wa Mwalimu, leo anaenda kinyume kabisa na misimamo yake wakati wa uhai wa baba wa Taifa.

Inaelezwa kwamba hasira na visasi vya Kingunge vinatokana na migogoro katika kampuni zake za ujenzi na ukusanyaji ushuru katika kituo cha mabasi na parking alikokuwa anainyonya serikali fedha ambazo zingeweza kutumika kulipia mishahara na huduma za hospitali.

Anatetea sas Biashara zake!,Watu wanaamini ni mkomonuisti lakini si kweli kwani sasa ni dhahiri Kingunge ni bepari… ana kampuni kazi za ujenzi na pia anahusika na kukusanya ushuru. Katika kutoza ushuru, iliwahi kubainika kwamba hata kiwango wanachopaswa kuwasilisha serikalini walikuwa wanakihujumu pamoja ya kuwa mkataba wenyewe ulikuwa tata. Waliidhulumu serikali amabyo mapato yake yalikuwa yaende kusaidia mishahara na madawa kwa hospitali za umma.

Kingunge anajenga chuki pia kutokana na kukosa msaada aliomba serikalini kumsaidia mmoja wa watu wa karibu naye aliyepata kesi nje ya nchi. Pia amekerwa na serikali kutaka utaratibu ufuatwe kwenye zabuni ya ukusanyaji ushuru na maegesho ya magari.

Tunajiuliza, Mzee Kingunge huyu ambaye alikuwa hamtaki kabisa Lowassa, na baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 alitaka sana kumzuia Lowassa asipewe Uwaziri Mkuu!?? Nini kimemfanya abadilike ghafla? Ni watu wake wa karibu kuwa katika timu ya Lowassa? Heshima ya Mzee Kingunge muda mrefu ilikuwa kwa kukitetea chama na serikali yake, inakuaje asubiri Nyerere aage dunia ndio abadilike
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: