1.Huna muda wa kushinda na mpenzi wako mkipiga stori za mapenzi.

2.Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unapofikiria ni kitandani.

3.Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe.

4.Mziki unaoupenda unausikia kwenye lifti au kwenye gari unapoenda na kutoka kazini.

5.Saa 11 alfajiri ndio muda unaoamka na siyo muda unaokuja kulala.

6.Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa.

7.Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda maisha club.

8.Ukienda kununua kitu Dukani unakuwa na juhudi kubwa za kuomba upunguziwe bei.

9.Idadi ya T-shirt na jeans inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo.

10.Wewe ndiye unayekumbuka kuwapigia simu polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wanaovuta bangi na kuwasumbua.

11.Ndugu zako watu wazima wanajisikia amani kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako

12.Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa.

13.wanyama uwapendao kama mbwa unawaandalia chakula kwa kufuata kanuni za kisayansi badala ya kuwapa mabaki uliyotoka nayo subways au steers.

14.Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana

15.Unaithamini sana ratiba yako ya kulala

16.Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulima lima bustani ya mboga mboga maua badala ya kutazama film au kuzurura mtaani

17.Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza kuuliza"umenunua shilingi ngapi?"

18.Unapokwenda Duka la Madawa unanunua ibuprofen na antiacid badala ya condom au kizuia mimba

19.Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi,nipashe,the express,majira,mawio badala ya kununua kiu,ijumaa,risasi au uwazi

20.Unapata kifungua kinywa kwa wakati

21.Ukiwa baa unanunua bia zinazokutosha badala ya kusema"zungusha kama tulivyo"

22.Asilimia 90 unayotumia kwenye kompyuta yako unatumia kwa shughuli badala ya kuchati

23.Ukimuona Rafiki yako mjamzito unampongeza badala ya kumuuliza"imekuwaje tena?"

24.Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja

25.Ukijisikia hamu ya kunywa unapunguza gharama kwa kunywea nyumbani badala ya kwenda baa

26.Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako

27.Ukiwa na Rafiki zako unapiga stori kuhusu mfumuko wa bei au mfumo mbovu wa utawala

28.Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa chumvi nyingi ama mafuta mengi

29.ukiona umefikisha nusu ya sifa nilizotaja wala hauhitaji kupigiwa kelele kwamba umri wako umeyoyoma!!!!!!!! shtuka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: