Ilikuwa ni majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo mzee mmoja mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 aliingia katika hospitali moja ili kusafisha kidonda chake mguuni.
Mzee akaanza kwa kuomba afanyiwe haraka kwa kuwa alikuwa na appointment ya muhimu sana ifikapo saa tatu kamili ya asubuhi hivyo afanyiwe msaada wa huduma ya haraka.
Daktari mmoja akaguswa na mzee yule baada ya kuona kila mara akiingalia saa yake na kutikisa kichwa cha kukatishwa tamaa, hivyo aliamua kumhudumia kwani alijua ingechukua zaidi ya saa kabla ya mzee kuhudumiwa kutokana na idadi kubwa ya watu kwa kuwa yeye hakuwa na mgonjwa wa kumhudumia wakati huo.
Baada ya uchunguzi wa kidonda chake kikaonyesha kuwa kimepona na daktari akaanza kukifungua akishirikiana na nesi kukisafisha.
Wakiwa wanaendelea na kukisafisha kidonda daktari na mzee wakaanza mazungumzo na daktari akamuuliza kama mzee alikuwa na appointment na daktari mwingine kwa jinsi alivyokuwa
na haraka.
Mzee akajibu hapana, ila anatakiwa kuwahi kwenda kunywa chai na mkewe ambaye alelazwa kwenye kituo cha kuhudumia wangonjwa wenye matatizo ya ubongo.
Mzee akaendelea kumwambia daktari kuwa mkewe amelazwa pale kwa zaidi ya miaka miwili akitibiwa maradhi hayo na hana kumbukumbu kabisa. Daktari akauliza sasa kama kapoteza kumbukumbu atakumbuka kama umechelewa???
Mzee akamjibu daktari kuwa mke wangu hajawahi kukumbuka kuwa mimi ni nani au nini kinaendelea kwa zaidi ya miaka hiyo miwili.
Kwa mshangao daktari akamuuliza, "Na umekuwa ukiendelea kwenda kunywa naye cha kwa miaka yote hiyo kila siku asubuhi hata kama amekusahau wewe ni nani?"
Mzee alitabasamu na kuushika mkono wa daktari na kumwambia "hanifahamu tena mimi, ila mimi bado namfahamu ni nani kwangu na umuhimu wake kwangu"
Daktari alifuta machozi huku akimtazama mzee yule akiondoka kulekea kwa mkewe kunywa chai kabla ya saa tatu kamili.
Daktari alijishika mikono yake kichwani na kusema, "Hii ndio aina ya mapenzi ninayoyataka katika maisha yangu"
Upendo wa kweli hauko kwenye mwonekano wa mtu au mapenzi. Mapenzi ya kweli ni kukubaliana na hali zote zilizopo, zitakazotokea na ambazo hazitatokea pia.



Toa Maoni Yako:
0 comments: