JAMII imeombwa kutoa msaada wa hali na mali kwa BI GRACE KAIZA mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye ameomba mukatwa mguu wake kutokana na Saratani ( Kansa) katika mguu huo.

Akizungumza jijini Mwanza, Bi. Grace Kaiza amesema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu jambo lililomuathiri kwa kiasi kikubwa kiafya na hata kiuchumi.

Akielezea namna tatizo hilo lilivyompata amesema lilianza kama uvimbe katika mguu wake kisha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini haikusaidia na ndipo alipobainika kuwa na ugonjwa huo.
Ameongeza kutokana na ugonjwa huo amekuwa akipata maumivu makali mno yanayo mliza hasa nyakati za usiku hali inayomfanya kushindwa kulala.
Fedha inayohitajika ili kuweza kumsaidia BI GRACE Aaondokane na tatizo alilonalo ni kiasi cha shilingi milioni mbili za kitanzania, ambazo zitamwezesha kuondolewa mguu kabla haujaleta madhara zaidi.
Kwa yeyote atakayeguswa na taarifa hii anaweza kuwasiliana na BI GRACE kwa ajili ya kumsaidia kupitia namba za simu 0768 264 182 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: