Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha Leonce Matley akikabidhi  misaada kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mtoto Afrika .
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha Leonce Matley akikabidhi misaada kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mtoto Afrika
---
JUKUMU la malezi ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu nchini linapaswa kutekelezwa na kila mtanzania pamoja na tasisi mbalimbali nchini ili kupunguza wimbi la wananchi tegemezi.

Hayo yalisema na Meneja wa Benki ya CRDb tawi la Meru, Leonce Matley, wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha St.Joseph kilichopo Kata ya Moshono jijini Arusha.

“Malezi ya watoto hawa yatima ni jukumu letu sote kama watanzania kuhakikisha kuwa tunawasaidia watoto yatimana wanaoishi mazingira magumu ili waweze kupata elimu bora itakayowakomboa kimaisha,” alisema Matley.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: