Kwa mara nyingine tena Yule msanii machachari ambaye anainukia kwa kasi katika muziki wa bongofleva Boniface( a.k.a handsome boy a.k.a asali ya Morogoro a.k.a bon-to-face) kwa mara nyingine tena ameachia wimbo na video yake mpya iitwayo “Nikitaka”. Audio ya wimbo huo umefanyika katika studio za Authentic Record jijini Dar es salaam chini ya Producer mwenye kiwango za hali ya juu Mr. Allan Mapigo, Video ya wimbo huu imefanywa kampuni mpya kabisa shine studioz, ni moja ya kazi safi kabisa chini ya Director matata kabisa Ivan. Boniface ni miongoni mwa wasanii wenye sauti nzuri na kujituma kwenye muziki, takribani ameshatoa nyimbo kadhaa siku za nyuma ambazo zimefanya vizuri sana nje ya nchi, Aidha, kwa sasa Boniface ameweka wazi kuwa hana meneja au msimamizi wa shughuli zake za muziki, kwahiyo milango ipo wazi kwa yeyote ambaye yupo tayari kufanya nae kazi za muziki kwa ujumla.

Wimbo : Nikitaka

Msanii : Boniface (Bon-To-Face)

Studio : Authentic Records

Producer : Allan Mapigo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: