Na Mwandishi Wetu

BONDIA Pius Kazaula wa Morogoro KG 66 amejitokeza hadharani na kuwaomba wadau wa mchezo wa masumbwi pamoja na mapromota kumwandalia mpambano kwa ajili ya kupima kiwango chake kwa kuwa mapromota wengi wapo Dar es salaam wao wa mikoani wanasahaurika.

Akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu amesema mabondia wa uzito wake wapo wengi ingawa kila siku wanapangiwa wao kwa wao maana unaweza kukuta bondia mmoja kacheza na mtu mmoja mara nne wakati mabondia wengine tupo mikoani tunafanya mazoezi tu bila kujipima viwango vyetu.

"Hivyo napenda kutoa wito kwa mapromota kujitokeza kutusapoti sisi mabondia wa mkoani ili nasi tujipime na mabondia mnao waamini,".

Bondia huyo mwenye makazi yake Morogoro hakusita kumpongeza kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sapoti anayotoa kwa mabondia mbalimbali na kuwapatia vifaa vya masumbwi kwa gharama nafuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: