Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania Julius Mcharo akiongea na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo waliohudhuria futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwenye hoteli ya Serena mwisoni mwa wiki.
 Baadhi ya wateja wa Benki ya CBA Tanzania wakipakua chakula cha futari iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye hoteli ya serena mwishoni mwa wiki
 Wateja wa Benki ya CBA Tanzania wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Serena Mwishoni mwa wiki .
.MkurugenzI na Maofisa waandamizi wa benki hiyo katika picha ya pamoja baada ya futari hiyo
---
Benki ya CBA Tanzania leo imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja ambapo pia itawaandalia wateja wake futari kwenye maeneo mbalimbali iliko na matawi nchini .

Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na CBA Tanzania kwa wateja katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Bw. Julius Mcharo alisema “ Tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii”.

Alisema Benki ya CBA Tanzania huwa inakutana na kushirikiana na wateja wake katika masuala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika matukio ya kuchangia kuinua sekta mbali mbali mfano afya na elimu. “Lakini leo ni siku muhimu kwetu hapa Dar es Salaam kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani ambao unaendelea”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: