Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Ernest Rwandalla akiwa na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi.
Akiwa na baadhi ya wasanii waliojitokeza
Akihojiwa na waandishi wa habari
Uzinduzi ulifanyika katika Bustani ya Wanyama ya Bahari Zoo iliyopo Tegeta
Mzee Chilo akiwa na mwigizaji Mkuu wa filamu hiyo.
Irene Paul nae alikuwapo pia kushuhudia uzinduzi huo
It was a happy day
Na Mwandishi Wetu


FILAMU Going Bongo ilizinduliwa rasmi juzi na kuhudhuriwa na mamia ya wadau wa filamu nchini, ulifanyika katika eneo la Bahari Zoo.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuizindua filamu hiyo, Mwigizaji Mkuu wa Going Bongo Ernest Rwandalla  alisema kuwa filamu hiyo imeshaanza kuoneshwa kimataifa zaidi kwa kuwa watu mbalimbali duniani wameanza kuifuatilia kwa njia ya I tune.

Alisema kuwa ni filamu ambayo inahusiana na suala la afya kwa hapa nchini ambapo inamuonesha mwigizaji kutoka Marekani ambae ni yeye akifanya kazi hapa nchini ya masuala ya Afya.


Alisema kuwa inaonesha ni kwa kiasi gani kuna thamani katika sekta hiyo na yeye akiwa kama mhusika mkuu ameamua kuigiza hivyo ili kuzionesha changamoto mbalimbali za sekta ya afya hapa nchini.

Alisema kuwa imetumia zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuikamilisha filamu hiyo na kuwa imehusisha wasanii mbalimbali wa ndani ya nchi pia.


Alisema kuwa imehusisha maeneo kama vile Kariakoo, Sinza na kwengineko huku mahala ambapo palikuwa pakitumiwa kama hospitali ni Mwananyamala.

Alisema kuwa kwa upande wake anaona kuwa kwa sasa kuna mafanikio makubwa katika sekta ya uigizaji hapa nchini kwa kuwa wasanii wengi wanaonesha hali ya kujituma na kufanya kazi yao kwa umakini zaidi.

" Going Bongo ni filamu ambayo inaweza kuandika historia mpya katika ulimwengu wa sanaa ya uigizaji kwa Tanzania kwa kuwa hadi sasa wapo watu wengi ambao wameanza kuiangalia filamu hii ndani na nje ya nchi" alisema.

Kwa upande wake mwigizaji mahiri wa filamu, Ahmed Olotu, Mzee Chilo ambae nae ameigiza kama mmoja kati ya wataalamu wa afya alisema kuwa filamu hiyo inaweza kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi.

" Hii ni filamu ambayo imeigizwa vema na ikiwa na kila umakini katika kuigiza na kuandikwa kwake na hata mpangilio wa habari ni mzuri pia" alisema Mzee Chiro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: