Waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na aliyewahi 
kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Joshua Kileo (Kulia)  baada ya ibada katika kanisa la KKKT Mjini Kati siku ya Jumapili.
---
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema  pamoja na mitihani mikubwa ambayo taifa inakabiliana nayo, umoja wa Watanzania utaifanya nchi isonge mbele kama taifa linalozingatia sheria na demokrasia.

Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili ya Pili ya Pasaka iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mjini Kati jana, Nyalandu alisema nchi itafanikiwa kupita mitihani hiyo kama wananchi wataimarisha umoja kati yao.

“Nchi inapita huku kukiwa na mambo mengi makubwa kufanya…kila mmoja anahitaji amani na hiyo tunaweza kuipata au  kufanikiwa kupita salama iwapo tutakuwa na umoja.

“Nchi yetu itasimama, itashinda mitihani ambayo tunayo kama ya uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu, upigaji wa kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” alisema.

Mapema katika mahubiri yake kanisani, Mteolojia Solomoni Dereva, aliwaomba Watanzania kuliombea taifa kwa Mungu ili liweze kupita kwa utulivu katika kipindi hiki chenye mambo makubwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: