Wewe  ni  dereva  wa basi la abiria ama  gari  binafsi? hebu  chukua  hatua ya  kupunguza ajali  leo kwa kujihadhari na  kona  hizi na Iyovi na Kitonga na  kona  nyingine kali kama  hizi nchini kwani maisha  yako ni  dhamani  kubwa na uhai  wake bado tunautamani.
 Vema  kuheshimu alama  za barabarani na  kuacha mbwembwe  uwapo  barabarani katika kona kali kama hizi.
 Katika kona  kama  hizi  zingatia  alama  za usalama  barabarani  usiwe na haraka  ya  kulipita gari la mbele

Kulipita gari la  mbele katika kona kama  hizi ni kutafuta ajali
Hapa  ni eneo ambalo watu 19 walipoteza maisha kwa fuso kugongana na basi na Nganga na kisha  kuwaka  moto uzembe  ukiwa ni wa dereva wa basi aliyetaka  kulipita gari la  mbele  katika  kona kali. 
 Usilipite gari katika  kona.
 Alama  zote  za barabarani ni msaada kwa maisha yako lazima uziheshimu.
 Kona zote ni hatari kwa usalama  wako hivyo usihame saiti yako ili  kukimbia ajali.
 Lazima  unapotaka kulipita gari la mbele uwe una uwezo wa kuona mbali  zaidi ya mita 100 ama  zaidi.
 Dereva makini halipiti gari  la  mbele katika  kona.
Kumbuka  ni  heri  kuchelewa ukafika salama kuliko kuendesha kwa haraka na ukafika majeruhi ama maiti tambua Taifa  linakuhitaji familia  inakuhitaji na  wewe  dereva ni msaada wa abiria  wote katika gari lako  na  msaada wa maisha yako jitambue, watambue abiria wako, jilinde utulinde  abiria  wako maisha  yako ni yetu na uhai  wako ni tegemeo letu epuka ajali zingatia sheria  za barabarani. 
IMETOLEWA NA MATUKIODAIMABLOG
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: