Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kumtangaza mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Mayunga Nalimi (katikati), katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia),
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akimkabidhi tuzo mwimbaji Mayunga Nalimi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia),
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akimpongeza mwimbaji Mayunga Nalimi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia),
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.
---
Mwakilishi kutoka Tanzania katika shindano la Airtel Trace Music Star Afrika Nalimi Mayunga ameibuka mshindi na kuwacha hoi washiriki wengine kutoka nchi 13 barani Afrika waliokuwa wakishindania kinyanganyiro hicho katika mashindano ya fainali za Afrika yaliyofanyika Naivaisha Kenya
Akimtangaza mshindi mwanamuziki nguli kutoka Marekani na jaji katika shindano hilo Akon alisema” Nimefurahisha sana na Mwanamuziki huyu chipukizi kutoka Tanzania kwani anao sauti nzuri iliyotulia na uwezo mkubwa wa kuiba. Mayunga ananikumbusha enzi zangu, na naamini akiendelea hivi na kupata mfunzo zaidi atafika mbali katika tasnia ya muziki. Naahidi kumpa mafunzo yatakayomsaidia kupata mbinu mbalimbali za kimuziki na kurekodi nyimbo nae moja, lakini akifanya vizuri ntampa zawadi ya kurekodi album pamoja nami”.
Akiongea katika halfa ya kumtangaza mshindi iliyofanyika high spirit, IT plaza jijini Dar es saalam Mkurugenzi wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” Shindano la Airtel Trace Music Star lilizinduliwa Oktoba mwaka jana, lengo likiwa ni kusaka, kukuza vipaji vya muziki na kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa kitanzania na Afrika kujulikana katika anga za muziki duniani.
Leo tunayofuraha kutimiza dhamira yetu kwa vitendo kwa kuwaweezesha watanzania kupata nafasi ya kushiriki na hatimaye moja kati yao kushinda. Nampongeza sana Nalimi Mayunga kwa ushindi huu na tunaamini nafasi hii ya kupata mafunzo na kurekodi na Akon utakuwa mwanzo wa safari yake ndefu ya mafanikio na kuzifika ndoto zake”.
Kwa upande Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza alisema “ Nachukua fulsa hii kumpongeza sana Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi yetu na kurudi na ushindi.
Nimefatilia mshindano haya yalikuwa ni na ushindani mkubwa sana, hii inaonyesha ni jinsi gani Tanzania tulivyo na vijana wenye vipaji lakini hawajapata nafasi ya kuvionyesha, nawapongeza sana Airtel kwa kuja na mashindano haya yanayowawezesha vijana wa kitanzania kupata fulsa ya kuonyesha uwezo wao na kufanikiwa zaidi.





Toa Maoni Yako:
0 comments: