Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope akipunga mkono kwa mashabiki pichani hawapo akiwa na mwenyeji wake Kulia amabaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) jioni ya jana tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka linalofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam, ambapo Solly Mahlangu mwanamuziki nguli mwingine wa muziki wa injili kutoka nchini humo atawasili leo na kujiunga moja kwa moja na tamasha hilo kushoto ni Mume wa Rebbeca.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayetambulika kwa jina la Rebbeca Malope akizungumza na vyombo vya habari mara baadaya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es salaam jana jioni.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope, akifurahia Skafu aliyovishwa na mmoja wa mwakilishi wa Msama Promotion.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope akiwa amepozi katika picha na Mwandishi wa Azam TV Timzoo Kalugira.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope, akiimba kwa furaha na akisema amefurahi kufika Tanzania na anaipenda Tanzania
PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA.


Toa Maoni Yako:
0 comments: