---
KIKUNDI cha kumsifu na kumwabudu Mungu cha Glorious Worship Team (GWT) katika Sikukuu ya Pasaka kilitoa burudani ya nguvu kwenye hafla ya kumsifu na kumwabudu Mungu iliyokwenda kwa jina la 'Mtoko wa Pasaka' na kufanyika Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo, GWT walimsifu na kumwabudu Mungu kwa nyimbo ikiwa ni muendelezo wa programu yao ya Sunday Celebration ambayo hufanyika kila Jumapili kuanzia saa 9 alasiri baada ya ibada.
Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa GWT, Emmanuel Mabisa amesema wiki hii katika Sunday Celebration Season 4 ndani ya Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mjasiriamali na Mtunzi mahiri wa Vitabu, Eric Shigongo ataendelea kutoa somo lake la Siri za kutoka kuwa Mwajiriwa hadi kuwa Mwajiri.
Katika somo hilo, Shigongo atatoa bure vitabu vyake zaidi ya 200 alivyoahidi kuvitoa kwa watu waliowahi kufika ukumbini katika Sikukuu ya Pasaka.
Waimbaji mahiri wakiwemo; Upendo Nkone, Carvary Band, The Jordan Moses Zamangwa (Mosax), na Masanja Mkandamizaji watakuwepo kutoa burudani siku hiyo ya Aprili 12, mwaka huu.


Toa Maoni Yako:
0 comments: