Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini jana kuhusu Mkutano Mkuu wa 31 wa ALAT utakaokwenda sambamba na Tuzo za Viongozi wa Serikali za Mitaa ‘Mayors Award’ na Miaka 30 ya ALAT, utakaofanyika katika hoteli ya Kunduchi jijijni Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo na (kulia) ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB ambao ndio wadhamini wakuu wa mkutano huo, Waziri Barnabas. PICHA NA JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG


Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 200, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi kwa ajili ya kudhamini mkutano huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo
---
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 31 katika hoteli ya Kunduchi jijijni Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Mkutano huo unaodhaminiwa na benki ya NMB ni “Wananchi pigia kura katiba pendekezwa kuboresha Serikali za Mitaa na maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015”“.

Mkutano mkuu wa 31 unafanyika pamoja na mambo makubwa mawili yafuatayo; Moja ni Sherehe za Miaka 30 ya Serikali za Mitaa na ALAT ambayo itakuwa na kongamano la kutathmini tulikotoka, tulipo na kuangalia nini cha kufanya huko mbeleni ili kuziwezesha Serikali za Mitaa kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. Pili, shaerehe za tuzo za viongozi bora wa Serikali za Mitaa (Mayors Award). 

Kwa mara ya kwanza ALAT itatoa tuzo kwa viongozi wa Halmashauri ambao wanafanya vizuri katika kusimamia Halmashauri zao. Katika mchakato wa kuwapata viongozi bora wananchi wameshirikishwa kwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwenda namba 15440.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: