Basi ndogo aina ya Coaster lililokuwa limebeba mashabiki wa Simba likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Shinyanga limepata ajali eneo la Makunganya barabara kuu ya Dodoma - Morogoro na kusababisha zaidi ya watu watano kufariki dunia papo hapo na wengine 19 kujeruhiwa mkoani Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:40 jioni baada ya utelezi uliosababishwa na kunyesha kwa mvua wakati mashabiki hao wakisafiri kwenda Shinyanga kuishangalia katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Kagera Sugar utaochezwa kesho kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Maiti ya ajali hizo wamehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro sambamba na majeruhi hao 19 kupatiwa matibabu.
Taarifa tulizozipata toka eneo la tukio japo Polisi bado hawajatoa tamko rasmi. Waliofariki ni mpaka sasa ni: Waluya, Rehema, Ali Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ Wabi na dereva wa gari Abdallah Fundi.
Mungu awalaze roho za marehemu mahala pema peponi na kuwapa unafuu majeruhi wote katika ajali hiyo.



Toa Maoni Yako:
0 comments: