Na John Badi wa Daily Mitikasi Blog, Dar es salaam.

MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwemo wanamuziki ‘kiduchu’ jana wameshiriki katika mazishi ya Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao katika makaburi ya Tegeta jijini. 

Baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo walionyesha kutoridhishwa na mahudhurio hayo kiduchu ya wanamuziki na kulaumu chini chini kuwa kukosekana kwa ushirikiano kati ya wasanii wa muziki nchini ndilo jambo linalopelekea tasnia kuporomoka kila kunapokucha.
Shughuli za mazishi zikiendelea. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG 

"Huenda mahudhurio haya kiduchu yanatokana na wengi kutopata taarifa mapema wengi wao wakifikiri huenda Marehemu Che Mundugwao angesafirishwa kwenda kuzikwa kusini” alisema mmoja wa wanamuziki wakonge hapa nchini ambaye hakutaka jina liwekwe katika mtandao huu. 

Aidha Daily Mitikasi Blog iliweza kuwashuhudia wanamuziki waliohudhuria msiba na mazishi hayo, kuwa ni pamoja Kiongozi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Luiza Mbutu, Kalola Kinasha na Ras Innocent Nganyagwa.
Viongozi wa Taasisi mbalimbali za sanaa nchini waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, Rais wa Muziki wa Rhumba Tanzania na mdau wa muziki nchini, Francis Kaswahili.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (wa pili kushoto), Ras Inno (wa pili kulia) na wadau wakiwa mazishini.
Mmiliki na Mhariri Mkuu wa Blog hii, John Badi (kushoto) akiwa na wadau wakati wa  mazishi katika makaburu ya Tegeta. Wa (pili kushoto) ni Kaka Bonda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: