Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la maendeleo ya Watu wa Marekani (USAID),Ana Bodibo–Memba akizungumza leo na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika viwanja vya Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa BG Tanzania,Stevenson Murray akizungumza leo na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika viwanja vya Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Afya ya Ifakara, Dk.Ladslaus Mnyone katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo hufanyika kila mwaka Aprili 25 yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imeitaka jamii kutumia vyandarua kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vyandarua hivyo vitumike kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki.
Hayo yamesemwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka.
Sadick amesema wafadhili mbalimbali wamekuwa wakiweka nguvu katika kupambana na Malaria hivyo ni wajibu jamii kutumia Vyandarua hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa kwani kufanya hivyo kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi kutokana na kuwa na afya iliyo bora.
Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo amezindua mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau mbalilmbali kupambana na ugonjwa wa Malaria.





Toa Maoni Yako:
0 comments: