Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akipokea msaada kutoka Kwa Mkurugenzi wa Duka la Dawa la Nakiete, Bi Batilda.
Duka la Dawa la Nakiete limetoa msaada katika hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya shilingi milioni 6.
Mkurugenzi wa Duka la Nakiete, Bi. Batilda amesema msaada huo ni faida waliyoipata kwa mwaka jana, hivyo wanarudisha sehemu ya faida hiyo kwa jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa wodi ya wazazi akimpa mmoja wa wakinamama waliojifungua jana sehemu ya zawadi zilizotolewa na Duka la Nakiete ambapo zaidi ya wakinamama 40 waliokuwa wamelezwa katika wodi hiyo walinufaika.
Baadhi ya wakina mama waliotembelewa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Makonda
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akishukuru kwa Msaada huo amewapongeza kwa moyo waliouonyesha wa kujitolea kwajili ya wananchi wenye uhitaji.
Aidha Mkuu wa wilaya amesema Nakiete wameonyesha mfano kwa kujitolea kwasababu wa Pamoja na kulipa kodi bado wameona umuhimu wa kujitolea kwa jamii ya tanzania tofauti na wachache wanaoikosesha serikali kwa kukwepa kodi na bado hata hawawakumbuki hata Wananchi maskini.

Toa Maoni Yako:
0 comments: