Watanzania na wakazi wa DSM, Kuna matukio ya unyanga'anyi kwa kutumia silaha na hata nguvu.

Matukio ya hayo yanatokea sana eneo lenye maduka makubwa Yaani super markets na maeneo yenye ATM na mabenki.

Wanowalenga sana ni wakina Mama na wageni kwa maana ya wazungu na watanzania wenye asili ya kiasia. Na mara nyingine hata wa akina baba wenye fedha.

Wanatumia pikipiki mbili ama moja na mara nyingine maeneo ya masaki na oysterbay ama mikocheni wanatumia magari ya zamani zamani kama corolla na saloon nyingine with a forged plate no.s.

Wanakuwa wengi ndani ya gari moja na mara nyingi hujifanya kama wana park gari ama wanakuuliza jambo huku waki target simu za mkononi na mifuko ya mkononi ya akina mama ama hao wageni wenye backpacks na brief case.

Hunyakua na kukuburuza na gari yao hata kilo meta moja bila kujali. Na matukio hayo mpaka sasa vyombo vya habari havitoi taarifa. Kuna wananchi wameumizwa na wengine kufa.

Kwa uoga wa watanzania hasa maeneo hayo ya masaki oysrterbay na mikocheni huwa watu wana sogea pembeni na kuangalia bila msaada wowote hata wa ku block magari na pikipiki hizo.

Wakijua kuwa wao ama wake zao ama watoto na other members of family hayatawatokea hayo bali hutokea kwa wengine.

Tuchukue tahadhari kubwa na kila mmoja ajilinde kwa vile hata huko masaki kwenye barabara 2-3 za kuingilia na kutokea wanafanya mchana kweupe na hakuna hatua zaidi ya geresha za hao wanaoitwa walinzi.

Usimuamini mtu kupita kiasi, walinzi , wauza magazeti na wapiga viatu dawa na vijiwe vya mitaani na habari zingine zinasema mpaka ma cashier wa ma benki ni informers wa hao wenye uhalifu huo.

Muda wote wako around the corners idle na ghafla hupokea simu ama message na kwenda kumuwahi dada anayetembea kwenye mtaa innocently na kuporwa daylight.

Chukua tahadhari jilinde na usisubiri kulindwa na mtu yeyote..

UJUMBE HUU WA TAHADHARI UTUMWE KWA WATU WENGI ILI KUKOMESHA MATUKIO YA KIHALIFU. TUJILINDE
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: