Tatizo moja ambalo linawakumba watu wengi, haswa vijana, ni ile akili ya kudhani unahitaji kuomba ruhusa sehemu flani au kwa mtu flani kabla haujafanya jambo kubwa duniani.
Kama unataka kupiga hatua na kubadilisha dunia, hamna form ya kujaza!
Maamuzi ni yako, na mtu pekee mwenye uwezo wa kukukataza ni wewe mwenyewe.
Unataka kuanzisha biashara? Anzisha!
Unataka kurudi shule uongeze elimu? Rudi!
Unataka kujenga nyumba? Jenga!
Maendeleo yanatafutwa na kila mtu, ila yanapatikana kwa wale ambao hata wakipingwa namna gani, hawakubali kushindwa.
Maamuzi ni yako. Unataka kufanya kitu, fanya.
Hamna fomu ya kujaza.



Toa Maoni Yako:
0 comments: