Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi 'Sugu' ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake mwingine utakaofanyika mei 30 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba ambapo atakabiliana na Keis Amal kutoka Mzazi GYM
Bondia huyo anayenolewa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ameingia kambini jana kwa ajili ya mpambano uho wa raundi sita ambapo siku hiyo mpambano mkubwa utakuwa ni kati ya bondia Fransic Cheka na Kiatchai Singwancha . kutoka
Thailand
Mpambano utakaokuwa wa raundi kumi promota wa mpambano uho Kaike Siraju aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ya kuvutia ambayo yatatajwa wakati ukifika
Hata hivyo amendelea kumkumbusha Cheka kuwa afanye mazoezi ya kutosha na akumbuke bondia anaekuja kucheza nae ni zaidi aliwo kutana nawo awali.


Toa Maoni Yako:
0 comments: