Meneja Masoko wa Access Benki, Jonas Muganyizi akieleza wakati wa uzinduzi wa Huduma Mpya ya Benki hiyo Ijulikanayo kama kwa jina la "RAHISI". Huduma hiyo inawawezesha Wateja wa Access Benki kupata huduma kwa njia ya Simu ya mkononi Access benki wamezindua huduma hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Selcom Tanzania. Ni Huduma rahisi inayowawezesha wateja kufanya mihamala popote na bila malipo yoyote.
 Mkutano ukiendelea kuwaeleza waandishi wa habari ubora wa huduma hiyo.

Mmoja ya wateja wa benki ya Access alisema faida za huduma hiyo humsaidia kupunguza kero za foleni kila mtu anajua, wala huitaji kupoteza muda mwingi kwenye hizo foleni kuanzia sasa, Access Bank imezindua huduma ya RAHISI.. hii ni rahisi kweli, kwa kutumia simu ya mkononi unaweza kutoa, na kuweka hela kwenye account yako ya Benki ya Access bila gharama yoyote.
 Wandishi wa habari wakiefuatilia kwa makini.
Meneja Mauzo wa Access Bank, Tabuley Njavike alisema mteja anaweza kufanya Mihamala Muda wowote na pia wateja wanaweza kufanya miamala Mingi zaidi bila kikomo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Roland Coulon akikata utepe kuzindua rasmi huduma Mpya ya Benki hiyo ijulikanayo kama RAHISI.
 Meneja Masoko wa Access Benki, Jonas Muganyizi akiwakaribisha wateja kuanza kutumia huduma hiyo rasmi mara baada ya kuzinduliwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Roland Coulon Akikata keki.
Wafanyakazi wa benki ya Access wakibadirisha mawili matatu mara baada ya uzinduzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: