Ajali ya Hiace imeua watu 24 eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Wadau Niko eneo la tukio, mpaka sasa miili 22 imefanikiwa kutolewa. Kwani Hiace hii ilidumbukia mtoni na bado miili miwili imenaswa, ndiyo inatolewa muda huu.

Watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. Ajali hii imetokea wakati Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria. Inaonekana ni ugeni Wa barabara, speed na gari kukosa break za kuaminika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: