Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Thabit Mwambungu akifungua rasmi kikao cha Uhamasishaji wa Mikopo ya Vifaa Tiba, Madawa, Vitendanishi na Uboreshaji wa Vituo.
Meneja wa NHIF mkoani Ruvuma Bw.Sylivery Mgonza akiwasisitizia wadau wa Afya mkoani Ruvuma kuchangamkia fursa ya Uhamasishaji wa Mikopo ya Vifaa Tiba, Madawa, Vitendanishi na Uboreshaji wa Vituo kutoka NHIF
Afisa kutoka NHIF makao makuu Bw. Isaya Shekifu akitoa mada kuhusu taratibu na vigezo vya kupata Mikopo hiyo katika zoezi la uhamasishaji mkoani Ruvuma.
Wadau wa Afya Mkoani Ruvuma wakisikiliza kwa makini mada katika uzinduzi wa uhamasishaji wa Mikopo ya Vifaa Tiba, Madawa, Vitendanishi na Uboreshaji wa Vituo.
Kutoka kulia Meya wa Manispaa ya Songea Bw. Charles Mhagama, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Daniel Malekela, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Thabit Mwambungu wakifuatilia mada mbalimbali katika uzinduzzi huo.
Picha ya pamoja ya Mh.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Wafanyakazi wa NHIF na wadau wa afya mkoani Ruvuma
---
*AWAPA MIEZI SITA WADAU WA AFYA MKOANI HUMO KUCHANGAMKIA MIKOPO HIYO)
Katika kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wake na watanzania kwa ujumla, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuanzia mwaka 2008 umekua ukitoa mikopo ya Vifaa Tiba na Ukarabati wa vituo vya kutolea matibabu.
Pia katika kuongeza juhudi za kutatua tatizo la dawa nchini Mfuko huu umeongeza mkopo wa Dawa na Vitendanishi kuanzia mwaka huu wa fedha 2014/2015 pamoja na mkopo wa vifaa vya Tehama ili kwenda na kasi ya ukuaji wa teknolojia.
Kutokana na mwamko hafifu wa watoa huduma za afya katika kuchukua mikopo hii Bodi ya wakurugenzi na Menejimenti ya Mfuko umeanzisha zoezi la uhamasishaji kuhusu umuhimu wa Mikopo hii.Zoezi hili linafanyika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.
Uhamasishaji huo umeanza rasmi mkoani Ruvuma na kuzinduliwa na Mkuu wa mkoa huo Mheshimiwa Thabit Mwambungu, mkutano huo pia ulihudhuriwa na wageni wengine kama Katibu tawala wa Mkoa, Mganga mkuu wa mkoa huo, Meya wa Manispaa ya Songea , Wakurugenzi wa wilaya, na watoa huduma kutoka vituo vya serikali na binafsi mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa wadau wa afya mkoani Ruvuma kuchangamkia fursa hii adimu na muhimu ili kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya mkoani humo."Haijawahi kutokea mkopeshaji akahamasisha wadau kukopa hivyo hii ni hali mpya katika wakati mpya hivyo natoa miezi sita tuchukue hatua na kuchangamkia fursa hii na ifikapo mwezi septemba 2015 nitahitaji ripoti ya tathmini", alisisitiza Mh.Thabit Mwambungu.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Meneja wa NHIF mkoani Ruvuma Bw.Sylivery Mgonza aliwasisitizia watoa huduma na wadau wa afya kuhakikisha wanatumia fursa hii ya mikopo kutoka NHIF ili kuboresha huduma na kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanachama wetu na watanzania kwa ujumla.







Toa Maoni Yako:
0 comments: