Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa pili kushoto na viongozi wa Halmashauri wakikabidhiana daraja la mto Kitewaka kwa ajili ya kujengwa kisasa baada ya serikali kukabidhi fedha za ujenzi huo Tsh miloni 240
Mbunge Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa kisasa.
Wannchi wa kijiji cha Maholong'wa wakimpongeza mbunge Filikunjombe kwa kutimiza ahadi yake.
Waumini wa kanisa la Anglikana Maholong'wa Ludewa wakimkabidhi zawadi mbali mbali mbunge Filikunjombe baada ya kuwasaidia bati na saruji ya kutosha kujenga kanisa jipya.
Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa wakiongozana na mbunge Filikunjombe mwenye kofia.
Mbunge Filikunjombe akisaidi kupalilia mahindi katika shamba la mchungaji wa kanisa la Anglicana Maholong'wa baada ya kufika kusaidia ujenzi wa kanisa hilo.
Mkutano wa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na wanakijiji wa Maholong;wa.
Mzee wa kanisa la E.A.G.T Maboga Ezekia Mhagama (kulia)akimwombea dua mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kutoa misaada mbali mbali ya ujenzi na kujitolea kinanda kwa kanisa hilo vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maholong'wa.
---
Na matukiodaima Blog.
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa daraja la mto Kitewaka katika kijiji cha Maholong'wa kata hiyo ya Ludende baada ya serikali kumpatia kiasi cha Tsh milioni 2480 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya ujezi wa daraja hilo .
Mbali ya kutimiza ahadi hiyo ya daraja pia amechangia vifaa vya ujenzi vyeye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Maholong'wa na ujenzi wa kanisa la Anglikana kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende wilayani Ludewa mkoani Njombe .
Akizungumza na wananchi hao leo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kuwepo bungeni ni heshima ya wana Ludewa na kuwa hata vurugu kubwa ambazo amekuwa akizifanya bungeni si kwa maana nyingine zaidi ya kupigania maendeleo ya wananchi wake.
Hata hivyo aliipongeza serikali kuwa kusaidia kutoa fedha hizo kwa wakati kwa ajili ya kuanza ujenzi hao na kuwa iwapo asingefuatilia kwa karibu serikalini ama angekuwa wa kulala bungeni yawezekana fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zisingetolewa sasa.
“Wapo wabunge wengine ambao kazi yao ni kusinzia tu na wala haulizi swali …..ila huo pia ndio uwakilishi wake ulipoishia …..mimi silali kule bungeni mimi ninawatetea na kuwapiganieni kwa kulia nalia na kwenye kugombana nagombana pia pale kwenye kunyenyekea nanyenyekea….. napenda kuwaelezeni kuwa kazi ambayo mlinipa kuwawakilisha bungeni naitumia vema hadi sasa sijakwama kuwatumikia ….nilisema mwanzoni mimi navurugu bungeni ila ni vurugu za kimaendeleo”
Filikunjombe alisema kuwa waakati akiomba kuwa mbunge wa Ludewa alitaka
wawakilisha bungeni na kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo hivyo angekuwa mbunge wa ajabu kama angekuwa mbali na shughuli za kimaendeleo katika jimbo lake.










Toa Maoni Yako:
0 comments: