Na Bakari Issa, Dar es Salaam.

Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Mohamed Matumla anatarajia kupanda ulingoni Machi 27 mwaka huu kupambana na bondia toka nchini China, Wang Xin Hua katika pambano la uzito wa Bantam litakalofanyika katika ukumbi Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo, Rais wa Shirikisho la Ngumi nchini (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustadh’ amesema wamemtafutia Mohamed Matumla pambano hilo kubwa la Kimataifa kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha bondia huyo katika michezo yake mbalimbali.

Aidha, Ustadh amesema Hall of Fame Boxing (HFB) wameamua kumleta bondia huyo toka nchini China kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Naye, Mkurugenzi wa Hall of Fame Boxing, ambaye ni promota wa pambano hilo, Jay Msangi amesema kabla ya pambano hilo kutakuwa na mapambano manne ya utangulizi na kuhudhuliwa na Rais wa Shirikisho la Ngumi duniani (WBF).

Kwa upande wake bondia atakaye panda ulingoni siku hiyo, Mohamed Matumla amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia bondia huyo anavyogaragazwa
Kutokana na kufanya maandalizi ya kutosha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: