Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto migogoro ya ardhi ambayo inatakiwa kila mtu ambaye amenyimwa haki ya ardhi watapata kutokana na utaratibu uliopo.

Makonda aliyasema hayo hivi karibuni wakati ziara ya kutembelea wilaya hiyo, Makonda alisema asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa maalumu kwa shughuli za jamii ni changamoto ya muda mrefu na natambua juhudi nyingi zilizofanyika katika kutatua.

Makonda alisema moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi zote muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye migogoro na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.

Alisema anatenga siku moja ambayo ni ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi na utaratibu huu utaanza machi 6 mwaka huu na zoezi la uandikishaji kwa wale wanaohitaji kusikilizwa matatizo yao utaanza majira ya saa 3.

Makonda alisema Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika katika kushughulikia matatizo hayo itaundwa na Katibu tawala wilaya (DAS) akiwa ni katibu, Mwanasheria wa Manispaa, Afisa Mipango miji, Afisa Ardhi.

Aidha alisema ili kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba wananchi wafuate utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya kufikisha kila muhusika ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali vinavyoweza kutumika katika kufikia uamuzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: