Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri. Kulia ni mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, jana kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri. 
Dkt. Bilal, akisalimiana na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, nchini Misri.
---
Mhe. Makamu wa Rais aliwasili jana na kupokelewa na mwenyeji wake.  Akifafanua kuhusu mkutano huo Dkt Bila alisema kuwa ‘’Misri ni wadau wetu katika maendeleo,  uhusiano kuwa mkutano huu utafungua fursa zaidi za uwekezaji baina ya nchi zetu. Mkutano huo wa siku tatu utafunguliwa baadaye leo na Rais wa Misri Abdel Fahah  Sisi, na kuhudhuriwa na baadhi ya wageni mashuhuri kutoka Mataifa mbalimbali akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje waMarekani, John Kerry.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: