Spika wa Bunge, Anne Makinda akizungumza katika wakati wa majumuisho ya ziara hiyo. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na Mkurugenzi wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka (MB) akiongea mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi ya Dege ECO Village iliyochini ya NSSF jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge.
Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipotembelea kukagua miradi ya shirika hilo likiwemo Daraja la Kigamboni ikiwemo mji wa kisasa wa Dege Eco Village.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi ya Dege ECO Village iliyochini ya NSSF jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge.
Wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge ikifuatilia kwa makini.


Toa Maoni Yako:
0 comments: