Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akikabidhi mkataba wa udhamini kwa Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka, katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam , ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.
Na Mwandishi Wetu.
Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kutoa msaada kwa walemavu kupitia kikundi cha walemavu kijulikanacho kwa jina la “Tunaweza Band”, kwa kuwawezesha kulipia gharama za kurekodi nyimbo zao mpya. Makabidhiano ya mkataba huo kati ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na Ontime Production yalifanyika katika ofisi za Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’ jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi, amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya kijamii ambayo kampuni imeazimia kuifanya kulingana na msimamo wa kampuni hiyo wa kuwa karibu na jamiii inayowazunguka. “Msaada huu ni sehemu ya azimio tuliloweka la kuwekeza katika jamii yetu inayotuzunguka. Watu wanaoishi na ulemavu husahaulika katika jamii na hawapati haki zote zinazostahili kwa binadamu. Haki za binadamu ni sawa kwa watu wote bila kujali ulemavu wao. Kukosa uwezo wa kujihudumia mwenyewe, huleta mateso kwa binadamu yeyote yule. Tunafurahi kuwasaidia wenzetu katika jamii hii kwa kuwapa uwezo wa kujiongezea kipato kutokana na vipaji walivyonavyo.



Toa Maoni Yako:
0 comments: