Nashukuru sana kwa kuendelea kunishika mkono hasa kwenye Non Stop Mixx zangu za kila mwezi, Mchango wako ni mkubwa sana.

Safari hii nimekuja na Mini Documentary ya dakika 8 inayoonyesha jinsi ninavyoziandaa Non Stop Mixx zangu, Pia changamoto gani ninazokutana nazo wakati naziandaa na ni watu gani ambao wako nyuma ya pazia wakati wa uandaaji.

Pia nimezungumzia safari yangu ya Nairobi Kenya na jinsi gani ambavyo nimeadvance hii idea yangu ya Mixx kwa mwaka 2015.

Kwa ushirikiano na vijana wenzangu wa IDEAL CONCEPTS,Bwana George Goyayi, Reginald Maro na Sadick Hamad tukatoka na kitu hiki ambacho tungependa watanzania wakione kupitia Blog au Website yako.

Asante sana na Mungu akubariki sana.

DAVID OMARI.
DJ D-OMMY.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: