Mwili wa baba mzazi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes ukiwa unaswaliwa nyumbani  kwa kaka wa marehemu maeneo ya Kawe jijini Dar jana mchana na baada ya kumaliza kuswaliwa hapo ulipelekwa msikitini na baada ya kutoka msikitini ulipelekwa kwenye makaburi ya Kisutu kwa ajili ya maziko.
 Mwili wa Ebby Sykes ukipandishwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda kuswaliwa baada ya kuswaliwa nyumbani kwa kaka yake eneo la Kawe jijini Dar
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes akiwa amepanda gari lililobeba mwili wa baba yake mzazi ili kuelekea msikitini kwa ajili ya kuswaliwa na kasha kupumzishwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar.
Baadhi ya wasanii pamoja na ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba wa marehemu Ebby Sykse.
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi ya msanii mkongwe,
Ebby Sykes yaliyofanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Waziri Mkuu mstaafu, jaji Joseph Warioba akiweka udongo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akiweka udongo katika kaburi la msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.
 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiweka udongo.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiweka udogo katika kaburi la mzee Ebby Sykes
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiweka udongo katika kaburi la mzee Ebby Sykes.
 Dully Sykes (wa pili kushoto) akiwa ndani ya kaburi la baba yake mzee Ebby Sykes wakati wa mazishi yake.
 Ndugu na jama wakishiriki mazishi.
Umati wa watu ukiwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya baba yake mzazi ambaye pia ni msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: