Katibu Mtendaji wa baraza la Taifa la Mitihani, Dk. Charles Msonde akitangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa Kidato cha nne, yaliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam.

Na Blasio Kachuchu wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezea kwa asilimia 10.8 huku shule za serikali za vipaji maalumu, kongwe na seminari zikiendelea kuporomoka na mwanafunzi wa kike kutoka Shule ya Sekondari ya Baobab mkoani Pwani, Nyakaho Marungu akiongoza Kitaifa.

Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji wa Wastani wa Pointi (GPA) ambao yanaonyesha shule 10 bora kitaifa zote ni binafsi huku mkoa wa Tanga ukitoa shule tano kati ya kumi za mwisho.
Bonyeza kusoma matokeo hapa; Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Shule za vipaji kama za Ilboru, Mzumbe, Msalato, Kilakala, Tabora Boys, Kibaha na Tabora Girls na Shule kongwe zinazomilikiwa na Serikali za Pugu, Zanaki, Bwiru Boys, Minaki, Azania na Jangwani kwa miaka ya hivi karibuni zimekuwa hazifui dafu mbele ya vipaji vingine kutoka shule binafsi.

Katika matokeo hayo ya Shule ya Sekondari ya Kaizirege ya mkoani Kagera imeongoza Kitaifa ambapo mwaka jana alikuwa ya kwanza kwa shule zenye watahiniwa chini ya 40.

Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema waliofaulu mtihani huo ni 196,805 sawa na asilimia 68.33 ya 288,247 ya waliofanya mtihani huo, ikilinganishwa na 235,227 sawa na asilimia 58.25 waliofaulu 2013.

Dk Msonde alisema wavulana waliofaulu ni 106,960 sawa na asilimia 69.85 na wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: