Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi nchini, John Kitime ameibukia katika filamu na karibuni amezindua sinema iitwayo ‘Kutakapokucha’ ambayo ina akisi watendaji wasio waadilifu wanavyozitumia vibaya ofisi za umma na kuchangia migongano katika jamii.

Katika filamu hiyo ambayo Kitime anacheza kama muigizaji mkuu, akitumia jina la Nongwa, ndiye mwanakijiji pekee ambaye nyumbani kwake kuna umemejua akijivunia televisheni wanayokuja kuiangalia na baadhi ya wakazi wenzake kijiji na huduma za kuchaji simu anazozitoa nyumbani kwake.

Kwa kutumia ofisi yake, anapora ardhi za watu na mbaya zaidi anawachukia wenye mwamko kidogo wa elimu ambao binafsi anaona hawana lolote zaidi ya kuhitaji kiti chake hali ambayo inazua migongano na migogoro mikubwa ambayo mwisho wake ndio kinachoifanya hiyo filamu kuwa na msisimko wa namna yake.

Filamu hiyo ambayo imeandikwa na Irene Sanga chini ya utayarishaji wa Sylone Malalo na kuongozwa na Simon Mwakifwamba, msambazaji mkuu ikiwa kampuni ya Proin Promotion, licha ya pia ina muigizaji mahiri nchini, Charles Magari ‘Mzee Magari’.

Mtayarishaji wa filamu hiyo, Malalo anasema movie hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu nchini na anawataka wale ambao wanapenda vitu tofauti kuangalia pia inashirikisha wasanii wa Sanaa za mapigano ‘martial arts’.

Magari ambaye anaigiza kama mtu ambaye anataka mabadiliko kijijini hapo na kuondokana na urasimu na ukiritimba wa Mzee Nongwa, ina waigizaji mahiri ambao pia ni walimu wa Sanaa katika Taasisi ya Sanaa (Tasuba) ambao ni na Thabit Hudu na Mwanaidi Zambo.

Filamu hiyo ni kazi ya kwanza pia ya mzalishaji Malalo ambaye amebobea katika utengenezaji wa picha za video, documentary na filamu mbalimbali za kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa ni katika jamii na baadhi ya filamu hizo ni pamoja na ‘Zawadi’ na zingine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: