Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM:

Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge Mheshimiwa William Lukuvi amesema kwamba serikali imejipanga kuendelea kuweka mazingira bora kwa vijana ili waweze kujiajiri wenyewe hali itakayosaidia kutatua tatizo la ajira nchini.

Mheshimiwa Lukuvi amesema hayo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kongamano la wajasiriamali vijana wanaosoma chuo lengo lilwa ni kuwapatia elimu kuhusiana na sula zima la kujiajiri wenyewe mara wamalizapo chuo na si kutegemea kuajiriwa serikali au katika kampuni mbalimbali nchini au nje ya nchi.

Waziri Lukuvi amesema kwamba serikali imeanza mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfuko wa vijana utakaotoa mikopo yenye masharti nafuu ana

Aidha Mheshimiwa lukuvi ametoa ushauri kwa walimu kuweza kutoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ili wanafunzi wakamaliza hapo wawe na muelekeo wa maisha wa kuanza kufanya ujasiriamali.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilgal walioandaa mkongamano hilo Peter Christopher amesema kwamba kongamano hilo limelenga kuwa saidia vijana ambao wanahitaji kujiendeleza kupitia ujasiriamali kuweza kupata fursa mbalimba za mikopo katika mabenki ili waweze kupata vyanzo vya kifedha ili kutanua na kuanzisha biashara zao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: