Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Kutokana na tatizo la Ujangili nchini kuendelea kila kukicha Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Razaro Nyalandu leo amezindua rasmi mkatakati wa Taifa wa kupambana na ujangili dhidi ya Tembo na wanyapori wengine pamoja na biashara haramu ya meno ya Tembo nchini.

Huo ni muendelezo wa kutafuta njia za kutokomeza ujangili ambapo hapo awali serikaili kupitia wizara hiyo imechukua hatua ya kuajiri askari wa wanyama pori 900 hadi kufikia Septemba mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Waziri Nyalandu amesema kwamba mkakati huo utasimamiwa na mamlaka ya wanyapori ambao wao watabeba jukumu hilo kwa asilimia 90.

Aidha mheshimiwa Nyalandu amesema kwamba wamejipanga kushirikiana na wizara zote nchini kusimamia na kupiga vita uhalifu dhidi ya wanyama pori ili vitendo hivyo ambavyo vinadumaza uchumi pamoja na utalii wanchi vimalizike.

Mkakati huo umefanya na serikali ya Tanzani kupitia wizara ya maliasili na Utalii kwa kushirikiana umoja wa mataifa kupitia UNDP Ofisi ya Dar Es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: