Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu akishudui uwekaji saini makubaliano kati ya Funiture Center DSM na Shirikisho la Mafundi Samani Tanzania (TAWOFE) tarehe 29 Oktoba, 2014 katika ofisi za Furniture Center Dar es Salaam. Makubaliano hayo, ni kuimarisha ushirikiano kwa kuingia ubia na wazalishaji wakubwa kama Furniture Center ili kunufaika na uwezo wao mkubwa kwenye maeneo muhimu kama mitaji, masoko ya bidhaa, teknolojia na vifaa vya kisasa vinavyofaa kutengenezea samani hizo.
Mhe. Nangu alisema, “ushirikiano wa namna hii utaboresha ununuzi wa bidhaa zinazopatikana nchini kwa urahisi na kukuza soko letu pia huu ni uzalendo wa hali ya juu uliooneshwa katika kuwawezesha mafundi samani kuingia katika soko la Kimataifa, wakijiamini kwamba bidhaa zao zina ubora wa Kimataifa na kupongeza uongozi wa Funiture Center DSM kwa hatua walioichukua”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: