Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh.Dkt. Christine Ishengoma akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa Tigo kanda ya kusini Bw. Jackson Kiswaga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kifurushi kipya cha tigo cha welcome pack mkoani Iringa, kifurushi hicho kitamwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakiak 20, mb175,sms bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.
Timu ya Mkoa wa Iringa iliyoshiki mashindano ya shimiwi ikiingia kwenye basi la Tigo la kidijitali kupata maelezo ya huduma zitolewazo na Tigo ndani ya basi hilo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa, hii ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dkt. Christine Ishengoma akipata maelezo toka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Tigo juu ya huduma zitolewazo ndani ya basi la kidijitali la Tigo kwenye uzinduzi wa kifurushi kipya cha Tigo welcome pack mkoani Iringa. Kifurushi inatoa muda wa maongezi wa dakika 20, mb175, sms bila kikomo na shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.
Msanii Lucas Mhavile maarufu Joti akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.
Msanii Slivery Mujuni maarufu Mpoki akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa waliofurika kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.
Msanii Joseph Haule maarufu Professor J akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa waliofurika kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: