JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anatangaza nafasi za kazi zifuatazo katika Idara ya Uhamiaji kwa Raia wote wa Tanzania wenye sifa.

1. KOPLO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya Tanzania

Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu).

A. SIFA ZA MWOMBAJI:
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 25 hadi 30.
(ii) Awe amehitimu kidato cha sita na kufaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili, Historia, Jiografia, Kifaransa, Hisabati ambapo masomo mawili kati ya hayo yawe katika kiwango cha “Principal”.
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
• Cheti cha Sheria;
• Cheti cha Kompyuta;
• Cheti cha Ufundi (FTC) kwenye fani ya umeme na mitambo
(iv) Waombaji wenye ujuzi wa mojawapo ya lugha zifuatazo (Kifaransa, Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza.
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa kipaumbele.

B. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kusimamia upangaji wa majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(ii) Kusimamia ufunguaji wa majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji pamoja na majalada binafsi ya watumishi wa uhamiaji;
(iii) Kuandika hati mbalimbali za uhamiaji;
(iv) Kuwa viongozi wasaidizi wa makundi ya doria na ukaguzi;
(v) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za uhamiaji mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini (Deportees)

4. ANUANI YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe kwa njia ya posta ndani ya kipindi cha siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa anuani zifuatazo:-
• Waombaji wa nafasi 200 (100 Koplo na 100 Konstebo) ambazo ni kwa ajili ya Tanzania Bara na Zanzibar wawasilishe maombi yao kwa anuani ifuatayo:

Katibu Mkuu, 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM.
• Waombaji wa nafasi 28 (14 Koplo na 14 Konstebo) ambazo ni maalum kwa Zanzibar wawasilishe maombi yao kwa anuani ifuatayo: Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
C/O Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
S.L.P 1354,
ZANZIBAR.
Maombi ambayo hayatazingatia maelekezo tajwa hapo juu hayatashughulikiwa.
CHANZO: DAILY NEWS LA TAREHE 29 SEPTEMBA 2014
---

2. KONSTEBO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya

Tanzania Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu).


A. SIFA ZA MWOMBAJI:
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 20 hadi 25.
(ii) Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili, Historia, Jiografia, Kifaransa, Hisabati ambapo masomo matatu kati ya hayo yawe katika kiwango cha “Credit”.
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
• Cheti cha Sheria;
• Cheti cha Utunzaji Kumbukumbu;
• Cheti cha Kompyuta;
• Cheti cha Ufundi (FTC);
• Cheti cha Mafunzo ya Ufundi Stadi kwenye fani ya (umeme, mitambo, bomba);
(iv) Waombaji wenye ujuzi wa mojawapo ya lugha zifuatazo (Kifaransa, Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza.
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa kipaumbele.

B. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kupanga majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(ii) Kufungua na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(iii) Kufanya doria sehemu za mipakani, bandarini, vituo vya mabasi, treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini;
(iv) Kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya uhamiaji na kuwafikisha kwenye mamlaka husika;
(v) Kufanya ukaguzi kwenye hoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara;
(vi) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za uhamiaji mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini (Deportees)
(vii) Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya uhamiaji;
(viii) Kuandaa hati mbalimbali za uhamiaji.

3. UWASILISHAJI WA MAOMBI
Barua za maombi zinapaswa kuandikwa kwa mkono na kuwasilishwa kwa njia ya posta zikiwa zimeambatishwa na:-
(i) Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
(ii) Nakala ya cheti cha kuhitimu masomo ya sekondari pamoja na vyeti kwa mujibu wa sifa nyingine zilizoainishwa kwenye kipengele A(iii). (result slips hazitakubalika)
(iii) Nakala ya vyeti vya kumaliza shule ya msingi na sekondari (Leaving Certificates);
(iv) Picha mbili (Passport Size);
(v) Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa/Shehia/ Vijiji;
(vi) Nakala za vyeti vyote vitakavyowasilishwa viwe vimethibitishwa na Wakili/ Kamishna wa Viapo.

4. ANUANI YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe kwa njia ya posta ndani ya kipindi cha siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa anuani zifuatazo:-
• Waombaji wa nafasi 200 (100 Koplo na 100 Konstebo) ambazo ni kwa ajili ya Tanzania Bara na Zanzibar wawasilishe maombi yao
kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu, 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM.

• Waombaji wa nafasi 28 (14 Koplo na 14 Konstebo) ambazo ni maalum kwa Zanzibar wawasilishe maombi yao kwa anuani ifuatayo: Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
C/O Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
S.L.P 1354,
ZANZIBAR.
Maombi ambayo hayatazingatia maelekezo tajwa hapo juu hayatashughulikiwa.
CHANZO: DAILY NEWS LA TAREHE 29 SEPTEMBA 2014
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: