Moja ya vijana wabunifu wa mavazi wanaozalisha bidhaa nzuri na kuziuza kimataifa ni Grabriel Mollel anayemiliki Kampuni inayoitwa Sairiamu Design aliyoianzisha toka mwaka 2009.

Ukiangalia bidhaa ambazo anazalisha ni nzuri kwa matumizi ya watanzania na zimekuwa zikiuza kimataifa.

Akizungumza na Kajunason Blog, Gabriel alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa jinsi anavyomjalia nguvu na akili ya kuendelea kubuni bidhaa ambazo Watanzania na watu wamataifa ya nje wamempokea vyema.

Alitaja nchi ambazo amekuwa akisambaza bidhaa zake ni Afrika Kusini, Sweden, Spain, Marekani kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki ni Kenya, Uganda na Rwanda.
Hivi ni viatu ambavyo amevitengeneza mbunifu Gabriel Mollel anayemiliki nembo ya Sairiam Design na huviuza nje ya nchi kutokana na ubunifu wake wa kutumia kitambaa cha nakshi ya masai shuka. Alisema moja ya jambo analolizingalia ni kutumia vifaa vyenye ubora na kushona kwa nadhifu tofauti na watu wengine ambao hubandika kwa gundi.
Viatu mahususi kwa wanawake.
Pundamilia...
Viatu vikiwa vimeshonwa kwa nakshi ya Khanga
Grabriel Mollel mnamo mwaka 2010 alifanikiwa kuingia katika Maonesho ya Swahili Fashion ambayo kwangu nahesabu kama ni moja ya mafanikio yangu.

Mwaka 2011 alifanikiwa kwenda Angola ambapo Swahili Fashion walinichagua tukiwa na Mustafa Hassanali, lakini vile vile Millen Magesse alitufanya sisi tukawa wageni maalum katika onesho la African Fashion Week la Afrika Kusini ambapo hapo nilijifunza mambo mengi sana.

2012 mwezi wa tatu alifanikiwa kwenda Kampala ambapo yeye mwenyewe ndiye alikuwa ‘Main Designer’, kwa sababu ma-designer wengine walionyesha nguo 10 lakini yeye alionyesha nguo 25, ikiwemo nguo moja wa ‘Ufukweni’ (Beach wear) na aliifanyia launch Kampala nchini Uganda.

Pia sasa anamiliki ofisi eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: