Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akikhutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola, ambapo aliwahimiza wananchi kujiunga kwa wingi kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii ili wawe wanapata tiba bora na familia zao kwa mwaka kwa kulipa sh. 10,000.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwapungia wananchi walipokuwa wakiingia kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola wakati wa zioara yao ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM tawi la Jegestal, alipoanza ziara wilayani Lushoto leo.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM tawi la Jegestal wilayani Lushoto leo. |
Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Henry Shekifu wakipiga makofi kufurahishwa na ngoma ya asili ya kabila la Wasambaa iliyokuwa inatumbuiza katika mkutano Mkuu wa majimbo ya Lushoto, Mlalo na Bumburi leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akipiga gitaa na kuimba wimbo uliotungwa enzi hizo na babake, Moses Nnauye wakati wa mkutano huo wa majimbo ya Lushoto, Mlalo na Bumburi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Kinana akitembelea bustani ya kuotesha miche ya miti katika Kijiji cha Kwesimu. Wilaya ya Kilosa imepanda zaidi ya miti milioni moja kwa ajili ya kuhifadhi mazingira. |
Kinana na Shekifu wakisaidia kupandikiza miche ya miti.
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Mbiwi, wilayani Lushoto.
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili eneo la mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Maji Marefu) akisalimia wananchi katika mkutano huo |
Nape akihutubia katika mkutano huo ambapo alishangazwa na tabia ya wapinzani ambao wameanza kutangaza sasa kuwa ajenda yao kuu kwenye chaguzi zijazo ni siual;a la katiba..
Nape akiunguruma katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola, Lushoto leo.
Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Henry Shekifu akielezea kwa wananchi kuhusu miradi mbvalimbal inayotekelezwa jimboni humo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mze Hoza Ismaili akimuomba Kinana amuarifu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete afanye ziara katika KLata ya Mlola kwani tangu walipotembelewa na Baba wa Taifa, Julius Nyerere enzi hizo hakuna rais mwingine aliyefika eneo hilo.
Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyewahi kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Lushoto kupitia NCCR Mageuzi, Deogratius Kisandu, baada ya kutangaza kujiunga na CCM katika mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments: