Mkurugenzi Mtendaji Panita, ndugu Tumain Mikindo akitoa nasaha zake kwa washiriki.
Washiriki wakiwa wanasikiliza hotuba kutoka kwa mgeni rasmi.
Mheshimiwa Mbunge, Lediana Mafuru Mungo'ng'o akielezea nafasi yake katika masuala ya lishe bora.
Mgeni rasmi Ndugu Charles Pallangyo akiwahutubia wageni waliofika katika warsha hiyo katika ukumbi wa Serena hotel jijini Dar es Salaam.

Ndugu Brenda Kaijuka, mshauri kutoka SUN akiwaelezea washiriki namna ya kuhamasisha lishe bora.

Na Mwandishi Wetu.

Watanzania, Asasi zisizo za serikali na wadau mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa mabalozi waLishe Bora katika jamii zinazo wazunguka, hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Ndugu Charles A. Pallangyo katika warsha ya siku 3 iliyofunguliwa leo tarehe 23 hadi 25 September 2014 katika Hotel ya Serena jijin Dar es salaam.

“Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara yake ya Afya na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imeendelea kuratibu masuala la lishe bora nchini, mfano mwaka 2013 serikali kupitia wizara ya afya imeanzisha kampeni nchi nzima yenye kuhamasisha lishe bora, na katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Lishe Tanzania (National Nutrition Implementation Plan) serikali imeajiri maafisa wa lishe katika Halmashauri takribani 147 na mikoa 20 huku ikiazimia kufikia halmashauri zote na Mikoa yote Tanzania Bara. Alisema Ndugu Charles A. Palangyo.

Aidha Katibu Mkuu aliweza kuzungumzia changamoto wanazokumbananazo katika kuhamasisha maswala ya Lishe bora nchini na kuwataka wadau, mashirika na Asasi zisizo za kiserikali kuendelea na mkakati huo.

“Pamoja na jitihada tunazozifanya , bado kuna changamoto katika zoezi zima la kuboresha lishe kwa watanzania, kwa mfano asilimia 42 ya watoto chini ya umri wa miaka 5 wamedumaa, asilimia 16 ya watoto hao wanaukondefu , na watoto wanaozaliwa na uzito pungufu wanakaribia kuwa asilimia 21.

Ukiachalia hilo, kwa upande wa kina mama, inakadiriwa kuwa asilimia 11 huwa wanakuwa na uzito pungufu, huku 53% ya wajawazito wanakumbwa na tatizo la upungufu wa wekundu wa damu.

 “Hivyo ningependa kuwaomba wadau, mashirika yaliyo bega kwa bega na serikali yaendelee kujitolea katika safari hii ya kuhakikisha kila mtanzania anapata lishe bora”, Aliongeza katibu mkuu Charles A. Palangyo.

Warsha hiyo ya kuhamasisha lishe bora katika jamii za kitanzania imefunguliwa leo na katibu mkuu wa wizara ya afya na ustwahi wa jamii katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam huku ikitazamiwa kufikia tamati tarehe 25 Septemba 2014.

Waratibu wa warsha hiyo ni shirikisho la SUN Movement Secretariat ambalo ni jumuhisho la nchi hamsini na nne (54) waliodhamiria kuboresha masuala ya lishe ndani ya jamii zao, ikishrikiana na Serikali ya Tanzania, PANITA pamoja na World Vision. Warsha hii inawashiriki kutoka nchi tisa Africa ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Nigeria, Zambia, Zimbabwe, Mozambique, Malawi na Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: