Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya Tigo Wekeza iliyozinduliwa leo kwa ajili ya kuwawezesha wateja wa Tigo Pesa zaidi ya milioni 3.5 kuweza kupata gawiwo moja kwa moja katika akaunti zao za Tigo Pesa. Kushoto ni Profesa Andrew Temu kutoka mfuko wa fedha Financial Services Deepening Trust (FSDT), wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson na wakala wa Tigo Pesa Ramadhan Wangwa.
Profesa Andrew Temu kutoka mfuko wa fedha Financial Services Deepening Trust (FSDT) akizungumzia ukuaji wa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu nchini. Profesa huyo pia aliipongeza Tigo kwa kuanzisha huduma hiyo mpya ya Tigo Wekeza ambayo itatoa gawiwo la zaidi kiasi cha shilingi bilioni 14.25 kwa wateja wake.
Wakala wa Tigo Pesa kutoka mkoani Dar es Salaam Ramadhan Wangwa akitoa ushuhuda wake kuhusu kuendesha huduma ya Tigo Pesa. Ukiondoa wateja wa kawaida, mawakala wakuu, mawakala wa kawaida nao watakuwa miongoni mwa wadau wa Tigo watakaopata sehemu ya gawiwo la shilingi bilioni 14.25.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,

Tigo Tanzania leo imekuwa kampuni ya kwanza duniani kuzindua huduma inayowapa watumiaji wa Tigo Pesa fursa ya kupata gawiwo la faida kwenye akaunti zao kulingana na kiwango fedha cha kilichopo.

Akitangaza uzinduzi wa huduma iitwayo Tigo Wekeza, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez amesema zaidi ya wateja milioni 3.5 wa Tigo Pesa watanufaika na malipo hayo ambayo yatatolewa mara nne kwa mwaka – kila baada ya miezi mitatu.

“Hii ina maana ya kwamba Tigo Pesa haitakuwa tena huduma ya kutuma na kupokea pesa tu kama ilivyo hivi sasa bali ni njia mojawapo kujipatia kipato cha ziada kupitia huduma ya Tigo Wekeza,” alisema Gutierrez.

Wiki iliyopita, Tigo ilitangaza kutoa gawiwo la shilingi bilioni 14.25 kwa wateja wake wa Tigo Pesa kutoka katika mfuko wa fedha ya akaunti ya Tigo Pesa, kitendo kilichoifanya kuwa kampuni ya simu ya kwanza duniani kutoa gawiwo kupitia huduma ya kutuma na kupokea fedha. Gawio hilo liliidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Julai mwaka huu.

“Tunatarajia kuona ongezeko la faida kutokana na uzinduzi huu wa huduma ya Tigo Wekeza ambayo tunaamini itakuwa kichocheo kwa wateja wengi zaidi kujiunga na kuanza kutumia Tigo Pesa kama sehemu ya kuhifadhi pesa zao pamoja na kutengeneza kipato. Aidha tunatarajia kuona ongezeko la watanzania kujiunga na mfumo wa fedha kitaifa,” alisema Meneja Mkuu huyo.

Kwa maelezo ya Gutierrez watumiaji wa Tigo Pesa watakuwa na nafasi ya kuchagua iwapo watataka kupokea au kuchangia gawiwo hilo kwa taasisi isiyo ya kiserikali, kutokana na sababu zao binafsi za kiutamaduni au kiimani. Ili kupata huduma ta Tigo Pesa. Mteja atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa neon “Wekeza” kwenda nambari 15514 ambapo atapata maelekezo zaidi.

Huduma hii mpya ni sehemu ya makakati wa kampuni ya Tigo wa kuendeleza matumizi ya kutuma na kupokea kwa njia ya mtandao wa simu, has kwa wananchi waliopo maeneo ya vijijini ambao hawafikiwi kirahisi nahuduma kutoka taasisi za kifedha.

Huduma ya Tigo Wekeza inakuja miezi sita baada ya Tigo Tanzania kushirikiana na Tigo Rwanda kuanzisha huduma ya kutuma fedha kati ya nchi hizo mbili. Huduma hii yenye mfumo wa kubadilisha fedha za kigeni za nchi hizo mbili ni ya kwanza ya aina yake duniani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: