Meneja wa mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha akiongea na Timu ya Taifa ya watoto mabaharia waliochaguliwa na shirikisho la mitumbwi midogo ya watoto Tanzania(TODA) itakayoshiriki mashindano ya wakimbiza mitumbwi yatayofanyika Agadir Morocco kuanzia tarehe 10 hadi 18 oktoba mwaka huu, Tigo ndio mdhamini wa safari hiyo.
Meneja wa mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha akipiga picha ya pamoja na Timu ya Taifa ya watoto mabaharia waliochaguliwa na shirikisho la mitumbwi midogo ya watoto Tanzania(TODA) itakayoshiriki mashindano ya wakimbiza mitumbwi yatayofanyika Agadir Morocco kuanzia tarehe 10 hadi 18 oktoba mwaka huu, Tigo ndio mdhamini wa safari hiyo.
Meneja wa mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kutangaza udhamini wa kampuni ya Tigo safari ya timu ya Taifa ya watoto waendesha mitumbwi inayoelekea nchini Morocco kushiriki mashindanoya wakimbiza mitumbwi mwezi ujao.
Mtoto baharia Max Pennanen Kok akionesha uhodari wake wa kuendesha mtumbwi kwenye fukwe za bahari ya Hindi maeneo ya Yatch club mtoto huyo ni mmoja ya watoto kumi watakaoshiriki mashindano ya wakimbiza mitumbwi nchin Morocco mwezi ujao, Tigo ni wadhamini wa safari hiyo.
Watoto mabahria wakiwa kwenye mazoezi na mitumbwi yao maeneo ya slipway kujiandaa na safari ya nchini Morocco mwezi ujao.

Na Mwandishi wetu.

Tigo Tanzania leo imetangaza udhamini wake kwa timu ya taifa ya watoto wadogo waendesha mitumbwi, timu ambayo inaundwa na mabaharia watoto 10 waliochaguliwa na shirikisho la mitumbwi midogo ya watoto Tanzania (TODA). Timu hii ya Taifa itashiriki mashindano ya 12 ya wakimbiza mitumbwi wadogo Afrika yatakayofanyika Agadir, nchini Morocco kuanzia tarehe 10 mpaka 18 Oktoba 2014.

Kukimbiza chombo hiki ni zoezi la kuendesha mtumbwi mdogo, kwa kawaida si zaidi ya urefu wa mita 6. Boti hii ya watoto wadogo ina urefu wa mita 2 na inafaa kwa ajili ya watoto wa chini ya umri wa miaka 16.

Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha alisema kuwa udhamini huu wa Tigo ni sambamba na dhamira ya kampuni hiyo kuwekeza katika kukuza vipaji vya wanamichezo nchini kuanzia wenye umri mdogo.

"Michezo inatambuliwa kama jambo muhimu si tu katika maendeleo ya vijana lakini pia katika kuunganisha vijana kutoka asili tofauti tofauti. Ni njia muhimu sana katika kuongeza kujiamini na kujifunza ujuzi upya. Ni makusudio yetu kuendeleza jitihada hizi za kuhamasisha mazingira ya michezo hapa Tanzania," alisema Wanyancha.

Aliongeza, "Tunaamini katika uwezo wa mchezo kuwawezesha vijana kutimiza malengo yao muhimu maishani. Sekta ya michezo inajenga fursa nyingi za ajira kwa vijana ambao wanatamani kutumia vipaji na ujuzi wao ili kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao.”

Mwakilishi wa nchi wa Shirikisho la mitumbwi midogo ya watoto Tanzania (TODA), Nelly Coelho, alieleza kuwa uendeshaji wa mitumbwi hii ya watoto ni mahsusi kwa ajili ya mabaharia vijana wenye umri kati ya miaka 8-15.

Aliongeza kusema, "Mabaharia waliofuzu wamekuwa wakipewa mafunzo kwenye ukingo wa bahari wa Msasani kutoka chama cha wamiliki wa majahazi, Dar es Salaam. Wengi wao walishawahi kushiriki katika mashindano mawili yaliyopita ya Afrika chini ya ufadhili wa Shirikisho la Mabaharia kwa kushirikiana kwa msaada wa vifaa vilivyotolewa na chama cha wenye Majahazi Dar es Salaam, ambao TODA inatoa shukrani nyingi kwao ."

Msaada wa Tigo umekuja kwa wakati mwafaka ambapo TODA ina mikakati ya kutangaza mbio za vyombo vya majini kama njia ya kuendeleza vijana. Mwakilishi wa TODA nchini amewashukuru Tigo kwa msaada huo na kuhimiza ushirikiano huo uwe endelevu.

Mashindano ya 12 ya watoto Afrika yameratibiwa kwa ushirikiano wa Shirikisho la Royale Marocaine de Voile na Shirikisho la kimataifa la Mitumbwi ya Watoto (TODA). Mashindano yatazileta pamoja nchi 13 barani Afrika ili kushindana kwa ajili ya michuano hiyo. Kila nchi mwanachama katika Afrika watapeleka mabaharia wapatao 10, waliofuzu katika majaribio ya Taifa. Pia TODA wanahamasisha kuwa kati ya hao mabaharia 10 katika timu angalau 3 wawe mabaharia wa kike ili kuhamasisha ukuaji wa vikosi kazi kwa wasichana. 

Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kupeleka wawakilishi wake kwenye tukio hili la kila mwaka kupitia Shirikisho la Mitumbwi midogo Tanzania (TODA). Tukio hilo lilifanyika mwaka 2005 na 2012, kwenye chama cha wamiliki wa Majahazi Dar es Salaam. 

Watoto watakaoenda nchini Morocco ni Alexandra Pennanen Kok(13),Savanna Desmarguest(13), Casey Deetlefs(12),Said Mkomba(13)
Hassan Mustafa(14), Vedastus Alphonce(14), Max Pennanen Kok(14), Friso Grolleman(12), Karim Jumanne(11) na Lenno Telemons(12)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: