Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar

Chama cha waandishi habari wanawake (TAMWA) kimezindua ripoti ya pili ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo Takwimu zimeonyesha kuwa matukio ya unyanyasi kwa mwaka huu yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Takimu hizo zimeonyesha uelewa wa wanachi katika suala zima la unyanyasaji wa kijinsia umeongezeka na wamekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa Taarifa kwa vyombo vya sheria.

Akizindua ripoti hiyo mwenyekiti wa Tamwa Rose Reuben amesema kwamba Utafiti huu ulifanyika katika wilaya kumi na ulilenga masuala yote ya ukatili wa kijinsia.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tamwa Gladness Munuo amesema kwamba kulingana na Takwimu zilizotolewa katika suala la ubakaji katika wilaya ya Unguja Magharibi Zanzibar umepungua ukitofautisha na miaka mingine ambapo katika wilaya ya Ilala Dar es Salaam kwa mwaka huu takwimu zimeongezeka ulinganisha na mwaka 2013.

Aidha Munuo amesema kwamba kuna changamoto kubwa katika wilaya ya Newala kwenye vituo vya afya kwa kuwa watoto wadogo njia za uzazi wa mpango ambapo bado itakuwa na kichocheo kikubwa cha watoto hao kupata virus vya ukimwi.

Rapoti hii ni ya pili ambapo Takwimu zinaonyesha kuna mabadiliko makubwa ya mafanikio katika Takwimu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: