Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' ametangaza kujiuzulu cheo hicho kupitia ukurasa wake wa instagram. Amedai kuna mpango mbaya dhidi yake hivyo akaona bora ajiengue.

Akizungumza na Kajunason Blog mara baada ya kuamua kufanya nae mahojiano kwa njia ya simu, Steve alisema amechoshwa na choko choko za watu ni bora akae pembeni aendelee na mambo yake mengine.

"Sina budi kusema basi, inatosha maana watu wenyewe ninao waongoza hawana shukrani maana nimewafungulia milango mingi ila kila kukicha ni kunisema vibaya, ehe! sina dhiki ya uongozo bora nijiengue.

Sasa nitaweka wazi mbichI na mbivu kesho katika mkutano na waandishi wa habari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: